Michezo

 
Dar es Salaam. Ndoto za Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil zilifutika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Ivory Coast.
Kwa matokeo hayo katika Kundi C,  Ivory Coast imefikisha pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine katika kundi hilo hivyo imeingia raundi ya tatu, wakati Morocco ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi nane wakati Tanzania ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi sita na Gambia inashika mkia ikiwa na pointi moja.
Taifa Stars imebakisha mechi moja dhidi ya Gambia itakayochezwa huko Banjul mwezi Septemba, pia Ivory Coast imebakisha mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa huko Abidjan.
Katika mechi jana, Taifa Stars ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 1 ambalo lilifungwa na Amri Kiemba kwa shuti kali la karibu akiwa ndani ya 18 baada ya mabeki wa Ivory Coast kusuasua kuondoa mpira wa tik taka uliopigwa na Mbwana Samatta.

No comments:

Post a Comment

 

Translate